Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

Mkutano wa Elimu na Uhamasishaji Mkoa wa Kigoma


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) hivi karibuni liliendesha Mkutano wa Elimu na Uhamasishaji kwa makundi mbalimbali ya jamii Mkoani Kigoma. Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea watumiaji uwezo wa kutambua haki na wajibu wao pamoja na fursa zilizoko katika sekta kwa lengo la kujiletea maendeleo.

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Esther Mahawe amelipongeza Baraza kwa juhudi zake zenye lengo za kumkomboa mtumiaji kifikra ''Nafarijika kuona Baraza limeipa Elimu kwa Umma na Uhamasishaji kipaumbele kwani ina uwezo wa kumkomboa mtumiaji wa huduma za mawasiliano kifikra, kimawazo na kimaadili.Hivyo basi; nilipongeze Baraza kwa kuweka mipango na mikakati mizuri ya kuimarisha elimu kwa watumiaji katika sekta hii ya mawasiliano inayokuwa kwa kasi na yenye mabadiliko ya haraka''

Aidha, Mkuu wa Wilaya Bi. Esther Mahawe alitoa rai kwa Watumiaji wa huduma za mawasiliano kutumia fursa zilizoko katika kujiletea maendeleo

''Nitoe wito kwa wananchi wa Kigoma kutumia fursa zitokanazo na huduma hizi kujiongezea maarifa, kupata taarifa mbali mbali za masoko, namna bora za uzalishaji mali, elimu na huduma nyingine muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kwa ujumla'' alisema Bi. Esther Mahawe

Akizungumza wakati wa kutoa salamu za Baraza, Katibu Mtendaji Bi. Mary Shao Msuya alieleza juu ya umuhimu wa washiriki kuendelea kutoa elimu watakayoipata kwa Watumiaji wengine ambao wanawakilishwa katika mkutano huo. Alifafanua kuwa lengo lingine la kufanya mkutano huo ni kuendesha uchaguzi wa wajumbe wa Kamati watakaochaguliwa na washiriki wa mkutano huo ili kusaidia katika jitihada za kupunguza kero na changamoto mbalimbali ambazo watumiaji wanakumbana nazo. Kamati hizo ni nyenzo muhimu itakayosaidia kuwafikia wanachi kwa ukaribu, kupata maoni yao na kuyawasilisha kwa Baraza kwa hatua zaidi.


Mkutano huo pia ulishirikisha wadau wengine wa sekta ya Mawasiliano wakiwemo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jeshi la Polisi na Watoa huduma za Mawasiliano ya Simu. Wadau hao walipata fursa ya kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusu sekta ya mawasiliano pamoja na kutolea ufafanuzi maswala mbalimbali yaliyoibuliwa na Watumiaji.

Tanzania Census 2022