Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Wajibu wa mtumiaji

Matumizi halali ya huduma

Ni wajibu wa mtumaji wa huduma za mawasiliano kuhakikisha kuwa anazingatia taratibu zote za kisheria na kanuni wakati wote ili kupata huduma zinazohusika.

Kutafuta habari.

Ni wajibu mtumiaji kutafuta, kusoma na kuelewa taarifa yoyote juu ya masharti na taratibu zinazohusiana na huduma au bidhaa anazotaka kutumia.

Kuchukua hatua

Mtumiaji ana wajibu wa kuwasilisha malalamiko kulingana na utaratibu uliowekwa endapo huduma au bidhaa haziridhishi au hazijafikia kiwango

Kulipia ankara

Ni wajibu wa mtumiaji huduma kulipia Ankara mara zinapotoka kwa kuzingatia taratibu na viwango vilivyowekwa.

Kulinda na kutunza miundombinu

Mtumiaji ana wajibu wa kulinda na kutunza miundo mbinu na vifaa vingine vya mawasilano ili kuwezesha upatikanaji endelevu wa huduma