Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Baraza

Muundo wa Baraza

Kifungu cha 37(1) V11 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003, kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya mawasiliano kuteua mwenyekiti na wajumbe wa Baraza.

Sheria inaainisha kwamba wajumbe wa Baraza hawatakuwa pungufu ya wajumbe saba na wasizidi idadi ya wajumbe kumi.

Wajumbe wa Baraza wanawakilisha makundi mbali mbali ya watumiaji yakiwemo Sekta binafsi, waishio kwenye mazingira magumu na vijijini na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Wajumbe wa Baraza ndio wasimamizi wa utekelezaji wa malengo na majukumu ya Baraza.

Wajumbe wa Baraza

Kwa sasa Baraza lina wajumbe saba (6) ambao ni:

1. Bw. Luckson Kataraihya - Mwenyekiti

2. Bi. Salma Abdallah - Makamu Mwenyekiti

3. Bw. Isaac Mruma - Mjumbe

4. Bw. Makange Mramba - Mjumbe

5. Bw. John Njawa - Mjumbe

6. Bi. Mary Shao Msuya - Sekretari wa vikao vya Baraza