Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Usajili wa namba za simu za mkononi

Kifungu cha 93(1) cha Sheria hii kinaainisha kwamba kila mwenye simu au anayetarajiwa kununua simu ya mkononi anawajibika kisheria kusajili namba yake. Kifungu hicho hicho cha 93(2) kinafafanua kila anayeuza sim card anawajibika kusajili namba ya simu kabla haijaanza kutumika.

Mabadiliko yoyote ya taarifa katika usajili wa sim-card yafanyike kwa mtoa huduma katika kipindi cha siku 15 tangu kutokea kwa mabadiliko hayo(96).

Usajili wa namba za simu za mikononi una madhumuni ya kumlinda mtumiaji na vitendo visivyofaa vinavyofanywa na watumiaji wengine mfano kutuma ujumbe wa vitisho, matusi na matendo ya kihalifu. Pia usajili unasaidia kumtambulisha mtumiaji na kumwezesha kupata huduma nyingine zinazotolewa kupitia simu za mkononi mathalani huduma za kibenki, kulipa ankara na ada za shule, kutuma na kupokea pesa na huduma za intanenti.

Masuala ya kuzingatia katika usajili wa simu

  • Mtumiaji anapaswa kutumia kitambulisho chake halisi na halali anaposajili sim-card
  • Ni kosa kisheria kutumia kitambulisho cha mtu mwingine katika usajili wa sim-card
  • Ni kosa kisheria kwa kampuni ya simu au wakala wake kumsajili mtu kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine

Vitambulisho vinavyotumika katika usajili wa sim-card

  • Hati ya kusafiria (passport)
  • Kitambulisho cha uraia
  • Kitambulisho cha kazi/shule/chuo
  • Kitambulisho cha benki
  • Barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa
  • Vitambulisho vingine vitakavyotolewa na mamlaka mbali mbali zinazotambulika kisheria