Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano

(TCRA-CCC)

Zingatia!!

  • Unapotuma vifurushi na vipeto hakikisha kwamba anaevisafirisha ana leseni halali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
  • Toa maelezo kikamalifu kuhusu vilivyomo ndani ya vifurushi au vipeto wakati unapovikabidhi kwa mtoa huduma kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kunapotokea kasoro katika kutoa huduma kama vile kupotea, kuchelewa au kuharibika.
  • Hakikisha maelezo haya yananakiliwa na unapewa nakala kwa ajili ya kumbukumbu zako.
  • Unapotuma vitu vya thamani kwa posta au kampuni ya usafirishaji wa vifurushi na vipeto hakikisha unapewa maelezo kuhusu haki zako iwapo kutatokea kasoro.
  • Iwapo utakumbana na matatizo kwenye utumiaji wa huduma na bidhaa za mawasilaiano, wasilisha malalamiko yako kwa mtoa huduma kwa maandishi, ukiweka wazi anwani yako na namba ya simu na tuma nakala TCRA-CCC na TCRA. Weka kumbukumbu za mawasiliano yote unayofanya kuhusiana na suala husika.