News
KAMATI YA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO MOROGORO WATOA ELIMU KWENYE MKUTANO WA WANAWAKE.
Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoani Morogoro yatoa elimu juu haki na wajibu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano na jinsi ya kutatua kero mbalimbali wanazokutana nazo watumiaji kwenye mkutano wa wanawake uliofanyika kata ya Uwanja wa Taifa Wilaya ya Morogoro Mjini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Samweli Msuya amesema kuwa wameelimisha kuhusu Sheria za Makosa Mtandaoni na kugawa vipeperushi vinavyohusiana na sheria za makosa ya mtandao,haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za Mawasiliano ikiwemo umuhimu wa kuripoti Makosa Jinai Polisi.
Aidha Clara Nkya Katibu wa Kamati ameongeza kwa kusema.''Elimu tunatoa kwenye vikao mbalimbali vya mitaa,mikusanyiko ya watu kama sokoni,maadhimisho ya sherehe mbalimbali,shuleni,mikusanyiko ya mpira wa miguu na maeneo mbalimbali ambayo yanakuwa na mikusanyiko ya watu kwakuwa ni rahisi kuwafikia katika makundi.’’Alisema Clara Nkya.
Aidha amesema mwitikio ulikua mzuri na wanawake hao walifurahi na kutaka wawe wanaelimishwa mara kwa mara kwakuwa wanakutana na changamoto nyingi wanapotumia huduma za mawasiliano ikiwemo utapeli na wanashindwa sehemu sahihi ya kuwasilisha changamoto zao.