Complaints Handling Procedures
UTARATIBU WA KUWASILISHA MALALAMIKO
Mtumiaji ambaye hakuridhika na huduma au bidhaa au ambaye amegundua kasoro katika matumizi anatakiwa kulalamika ili suala husika lifanyiwe kazi na kupatiwa ufumbuzi.
Malalamiko ni Nini?
- Malalamiko ni hoja ambazo zinawasilishwa na mtumiaji kwenye ngazi stahiki kutokana na kasoro au kutokukamilika kwa huduma au bidhaa husika. Mtumiaji anatakiwa kulalamika badala ya kunung’unika ili kupata ufumbuzi wa changamoto zinazo mkabili.
- Mtumiaji atawasilisha malalamiko yake kwa utaratibu ufuatao:- Sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Kanuni za Kumlinda Mtumiaji vimeainisha utaratibu wa kuwasilisha malalamiko. Utaratibu huu una hatua nne ambazo ni: -
Kuwasilisha Malalamiko kwa Mtoa Huduma
- Hii ni hatua ya kwanza na ya muhimu kwenye mtiririko wa kuwasilisha malalamiko. Mlalamikaji anatakiwa kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake na kuweka kumbukumbu ya malalamiko yake kwa maandishi.
- Endapo baada ya siku 30 Mtumiaji hajajibiwa au hajaridhika na majibu ya Mtoa huduma, anatakiwa kuwasilisha rufaa ya malalamiko yake Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Kuwasilisha malalamiko Kitengo cha Malalamiko Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA)
- Mtumiaji anapowasilisha malalamiko TCRA anatakiwa kuambatanisha nakala ya mawasiliano ya barua au barua pepe kati yake na mtoa huduma wake, pamoja na vielelezo vingine vyovyote vinavyohusu shauri husika na kutatuliwa kwa njia ya mashauriano. Iwapo mtumiaji hataridhirika na usuluhishi, atawasilisha malalamiko yake Kamati ya Malalamiko:
- Baada ya kupokea malalamiko, Kamati itawaita pande zote na kuzisikiliza na itatoa uamuzi ndani ya siku 30 hadi 60. Upande ambao hauridhiki na uamuzi wa Kamati, unaweza kukata rufaa kwenye Tume ya Ushindani wa haki kibiashara (Fair Competition Tribunal FCT). Malalamiko yanayohusiana na maudhui ya utangazaji yatasikilizwa na Kamati ya Maudhui.
Kukata rufaa kwa Tume ya Ushindani wa Haki (Fair Competition Tribunal (FCT).
- Upande ambao haukuridhika na uamuzi wa Kamati ya Malalamiko au Kamati ya Maudhui unaweza kukata rufaa kwenye Baraza la Ushindani wa Haki Kibiashara (Fair Competition Tribunal - FCT) ndani ya siku 21 baada ya kupokea uamuzi wa Kamati