Consumer issues
Masuala muhimu ya kuzingatia
Kuwa Makini Wakati Unachagua mtoa huduma
- Fanya utafiti, linganisha kuhusu gharama, ubora wa huduma na upatikanaji wa huduma au bidhaa
- Tembelea ofisi za watoa huduma ili kupata maelezo,
- Soma machapisho ya watoa huduma, tembelea wavuti wa mtoa huduma au uliza wanaotumia huduma hizo kwa wakati huo kuhusu uzoefu.
- Soma mkataba na maelezo ya mtaoaji wa huduma
- Hakikisha unaelewa masharti ya huduma husika kabla ya kujiunga; zikiwemo gharama na wakati wa kulipia
- Pale ambapo vipeperushi vinasema “vigezo na masharaiti kuzingatiwa ” ulizia kwa kina upewe hivyo vigezo na masharti yenyewe kabla ya kujiunga na hiyo huduma.
Kuwa makini unaponunua vifaa vya mawasiliano
- Unaponunua vifaa vya mawasiliano kama simu , redio, televisheni, ving’amuzi hakikisha
- Unanunua kwa wakala aliyeidhinishwa
- Unapewa risiti halali
- unapewa garantii ya si chini ya miezi 12 kwa maandishi,
- Unapewa karatasi ya maelezo ya kukitumia angalau yakiwa kwa lugha ya kiingereza au Kiswahili na kifaa hicho kiwe ndani ya kasha la kifaa hicho.
- Usipeleke kifaa chenye gerentii kwa fundi mwingine kama hakifanyi kazi kabla ya muda wa gerentii kumalizika.
Wakati wa kutumia
- Hakikisha kwamba huduma unayotumia inaendana na maelezo uliyoyapata awali wakati wa kununua; kwa mfano bei, utoaji wa taarifa muhimu na kadhalika.
- Tunza kumbukumbu za mkataba/maelekezo ya awali zikiwemo nyaraka kama risiti, fomu za usajili, kijitabu cha maelezo na karatasi ya gerentii