News
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aahidi ushirikiano kwa Kamati ya Watumiaji Mkoa wa Simiyu
Simiyu.
Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Simiyu (RCC) Oktoba, 10 2024 imekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenan Laban Kihongosi kwa lengo la kujitambulisha kwake na kufanya mashauriano ya kushirikiana na Serikali katika Mkoa wa Simiyu katika kuelimisha, kuhamasisha na kukusanya maoni ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano katika Mkoa wa Simiyu na kuwasilisha kwa Baraza kwa hatua zaidi.
Kwa upande wake, Mhe. Kihongosi, aliahidi ushirikiano wa dhati na kushirikisha Kamati katika shughuli mbalimbali za kiserikali na mikitano yake ili Kamati ya Watumiaji Mkoa wa Simiyu iweze kuongeza ufanisi katika kutoa elimu, kuhamasisha na kupokea maoni ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.
Sambamba na hayo, Oktoba 11, 2024, Kamati ya Watumiaji Mkoa wa Simiyu imetoka elimu ya matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano pamoja na Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni katika siku ya maadhimisho ya Mtoto wa kike duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Takribani wanafunzi 2980 walishiriki ikiwa ni Shule za Msingi na Sekondari kutoka Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Aidha; tukio hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, na wadau wa elimu ili kujadili na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili watoto wa kike katika mkoa huo.