Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

TCRA CCC Yatoa Elimu ya Usalama Mtandaoni kwa Walimu na Wanafunzi wa Sekondari Chenge Mkoani Simiyu


Katika kuendeleza juhudi za kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi salama ya huduma za mawasiliano, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA - CCC), kupitia Kamati ya Watumiaji Mkoa wa Simiyu, limeendesha mafunzo kwa wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Chenge iliyopo Kata ya Somanda, Bariadi Mjini.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uelewa walimu na wanafunzi kama watumiaji wa simu janja kuhusu matumizi sahihi ya mtandao, huku yakisisitiza namna ya kujiepusha na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika matumizi ya mtandao.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na utapeli wa mtandaoni, unyanyasaji wa kimtandao, usambazaji wa jumbe za uongo na uchochezi, pamoja na ulinzi wa taarifa binafsi na usalama wa watoto mtandaoni.

Jumla ya washiriki 415 walihudhuria mafunzo hayo, wakiwemo wavulana 220, wasichana 186, na walimu 9.

Akizungumza katika tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji Mkoa wa Simiyu, Ndugu Faustine Juma Gomu, alisisitiza umuhimu wa kuwajengea wanafunzi uwezo wa matumizi sahihi ya mitandao ili iwasaidie katika maendeleo yao ya Kielimu.

“𝑈𝑙𝑖𝑛𝑧𝑖 𝑤𝑎 𝑡𝑎𝑎𝑟𝑖𝑓𝑎 𝑏𝑖𝑛𝑎𝑓𝑠𝑖 𝑛𝑖 𝑚𝑠𝑖𝑛𝑔𝑖 𝑤𝑎 𝑢𝑠𝑎𝑙𝑎𝑚𝑎 𝑚𝑡𝑎𝑛𝑑𝑎𝑜𝑛𝑖, 𝑛𝑎 𝑤𝑎𝑛𝑎𝑓𝑢𝑛𝑧𝑖 𝑙𝑎𝑧𝑖𝑚𝑎 𝑤𝑎𝑒𝑙𝑖𝑚𝑖𝑠ℎ𝑤𝑒 𝑘𝑎𝑏𝑙𝑎 ℎ𝑎𝑡𝑎𝑟𝑖 ℎ𝑎𝑖𝑗𝑎𝑤𝑎𝑓𝑖𝑘𝑖𝑎 𝑖𝑙𝑖 𝑤𝑎𝑗𝑒𝑛𝑔𝑒 𝑡𝑎𝑏𝑖𝑎 𝑠𝑎𝑙𝑎𝑚𝑎 𝑦𝑎 𝑘𝑢𝑡𝑢𝑚𝑖𝑎 𝑚𝑡𝑎𝑛𝑑𝑎𝑜 𝑘𝑤𝑎 𝑚𝑎𝑒𝑛𝑑𝑒𝑙𝑒𝑜 𝑦𝑎 𝑘𝑖𝑒𝑙𝑖𝑚𝑢 𝑛𝑎 𝑘𝑖𝑗𝑎𝑚𝑖𝑖 𝑘𝑤𝑎 𝑢𝑗𝑢𝑚𝑙𝑎.” alisema Ndugu Gomu.