Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

TCRA CCC: Wanafunzi Msiharibu Kesho Yenu kwa Matumizi Mabaya ya Mitandao ya Kijamii.


Kusini Unguja📍

Wanafunzi nchini wametakiwa kuitumia vyema mitandao ya kijamii ili kuijenga kesho yao na si kuiharibu kwa vitendo visivyofaa mtandaoni.

Akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha Kwanza hadi cha Sita katika Skuli ya Sekondari Hasnuu Makame Mkoa wa Kusini Unguja, Mwenyekiti wa Kamati ya Watumiaji mkoani humo Maryam Haji Ramadhan amesema matumizi mabaya ya mitandao yameharibu 'future' ya Vijana wengi nchini.

"Leo unaweza kuchati na Mtu mtandaoni humjui, anakurubuni, anakufanyia vitendo vya kikatili. Nawasihi sana someni kwa bidii, social media mtazikuta tu mkifika Chuoni," amesema Maryam Haji.

Kwa upande wake Uongozi wa Skuli hiyo umelishukuru Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano nchini - TCRA CCC kwa kutoa Elimu kuhusu Ulinzi wa Mtoto mtandaoni kwani itawasaidia Wanafunzi kuripoti haraka vitendo hivyo wanapokutana navyo.

TCRA CCC imeendelea na Kampeni ya Ulinzi wa Mtoto mtandaoni ikiwa ni Kampeni Maalum kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Juni 16 mwaka huu.