Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

Wanafunzi Lindi Waelimishwa Kuhusu Matumizi Sahihi ya Huduma za Mawasiliano.


Kamati ya Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano mkoa wa Lindi imeendesha mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lindi, wakiwemo wale waliomaliza mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka 2024.

Mafunzo haya ni muhimu sana katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Mafunzo yamelenga kusaidia wanafunzi kutambua haki na wajibu wao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na kujitegemea kama watu wazima.

"Elimu hii imelenga katika kuwaanda wanafunzi, hasa wanaomaliza kidato cha nne, kuwa raia wema na wenye maadili katika matumizi sahihi ya huduma na bidhaa za mawasiliano kwani pindi wakiwa shule hawaruhusiwi kutumika vifaa hivyo," alisema Prisca Unga, Mjumbe wa Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Lindi.

Wanafunzi wamejifunza kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, usalama mtandaoni, na fursa zilizoko katika sekta ya mawasiliano. Mafunzo haya yanatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwa vijana hawa katika kuhakikisha wanakuwa watumiaji bora wa huduma za mawasiliano.

Katika muktadha wa mafunzo haya, elimu juu ya mawasiliano ni sehemu ya mwendelezo wa utoaji wa elimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini Tanzania. Mafunzo haya yanaimarisha uwezo wa vijana katika matumizi sahihi ya teknolojia, hivyo kuchangia kuimarisha maadili na usalama katika jamii.