Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO LAWATAKA WATUMIAJI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHUMI WA KIDIJITI.


BARAZA LA USHAURI LA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO LAWATAKA WATUMIAJI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHUMI WA KIDIJITI.

Baraza la ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano limeshiriki maonesho yaliyofanyika katika mkutano wa 41 wa Umoja wa Mashirika ya Posta Afrika (PAPU),yenye lengo la kutoa elimu kwa watumiaji kuhusu sekta ya mawasiliano hasa huduma za Posta na kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa sekta kutoka nchi za Afrika.

Hilary Tesha Mkuu wa Idara ya Elimu kwa mtumiaji Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano akizungumza akiwa Jijini Arusha amesema licha ya kuwepo kwa mkutano huo na shughuli nyingine pia yameandaliwa maonesho kuanzia tarehe 30 Agosti hadi Septemba 1, 2023 ambapo Tarehe 2 Septemba Mhe. Rais amezindua Jengo la Makao makuu ya Umoja wa Mashirika ya Posta Afrika Jijini Arusha.

Aidha Tesha amesema kuwa Baraza limeona ni vyema kushiriki maonesho hayo kwakuwa ni nafasi ambayo mtumiaji anauwezo wa kukutana moja kwa moja na Baraza kuleta malalamiko na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika matumizi ya huduma za mawasiliano.’’Watumiaji wategemee kuendelea kupata elimu zaidi, na maoni yao Baraza litawasilisha kwa Serikali na watoa huduma.’’Alisema Hilary Tesha.

Mkuu huyo wa Idara ya Elimu kwa Mtumiaji TCRA CCC, ametoa rai kwa watumiaji washiriki Kikamilifu katika uchumi wa kidijiti ambapo kupitia huduma za posta na mifumo ya anuani zinarahisisha na kuchagiza maendeleo ya uchumi wa kidijiti.