Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

BARAZA LAHUDHURIA KONGAMANO LA CONNECT 2 CONNECT (C2C).


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano limehudhuria Kongamano la “Connect 2 Connect (C2C)” lililofanyika Zanzibar Lengo kuu la Kongamano lilikuwa ni kujadili changamoto na njia za kutatua matatizo katika sekta ya mawasiliano ya kidigitali barani Afrika.

Tumaini Magila Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC), amewakilisha Baraza katika mkutano huo ambapo tarehe 6 Septemba 2023, Kongamano hilo lilifunguliwa na Mheshimiwa Khalid Suleiman Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). na tarehe 7 Septemba 2023, lilifungwa kwa hotuba nzito kutoka kwa Mheshimiwa Nape Nnauye (Mb), Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari.

Magila amesema katika kongamano hilo baraza limepata nafasi ya kuchangia hoja ni namna gani TCRA CCC inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha mawasiliano ya kidigitali yanaimarishwa na yanawanufaisha wadau wetu.“Ikumbukwe kwamba,baraza ni mdau muhimu katika kuhakikisha changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi kwa lengo la kuboresha na kumnufaisha mtumiaji wa huduma za mawasiliano’’.Alisema Tumaini Magila.

Kongamano la “Connect 2 Connect (C2C)”lilijikita katika kuimarisha Ushirikiano na mijadala ya kina ikiwa ni sehemu ya kufikia suluhisho bora na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano ya kidigitali barani Afrika.