News
Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Yatoa Elimu Mkoani Tabora
Tabora
Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Tabora imefanya mkutano wa kuelimisha na kuhamasisha vijana wa Kanisa la FPCT-Ipuli mkoani Tabora tarehe 29 Agosti 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo hayo, mwakilishi wa Kamati hiyo alisema kuwa lengo kuu ni kuwaelimisha vijana kuhusu masuala muhimu yanayogusa maslahi ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano.
Masuala hayo ni pamoja na haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano, matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, pamoja na ulinzi wa taarifa binafsi ili kujikinga na utapeli na uhalifu wa kimtandao.
Katika mafunzo hayo jumla ya vijana 33 walishiriki, ambapo kati yao walikuwa wasichana 20 na wavulana 13. Vijana hao walionyesha kuridhishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kuitumia katika maisha yao ya kila siku.
Naye mwenyekiti wa Kamati ya watumiaji ya Mkoa wa Tabora amesema kuwa kamati hiyo itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini, shule na makundi mbalimbali ya kijamii kuhakikisha elimu ya ulinzi wa mtumiaji inafika kwa wananchi wote. Alisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtumiaji anapata huduma bora na anafahamu haki zake


