Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Yatoa Elimu Shule ya Msingi Kagera Mkoa wa Kigoma


Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano imefanya kampeni ya kutoa elimu kwa wanafunzi katika Shule ya Msingi Kagera iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Mada kuu ililenga kuelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na Kufahamu haki zao Kama watumiaji Wa huduma za mawasiliano.

Aidha; Kamati imewataka wanafunzi hao kusambaza elimu hiyo kwa wazazi na walezi wao ili kuepuka changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi yasiyo sahihi ya huduma za mawasiliano.

Akizungumza na wanafunzi hao, katibu wa Kamati bi. Bertha mshana alisema "Wanafunzi kama walivyo watumiaji wengine wanaweza kukumbwa na changamoto kama vile udhalilishaji, utapeli au kuibiwa taarifa binafsi ka kutumika vibaya na watu wasio na nia njema, hivyo ni muhimu kwa elimu hii kuwafikia" alisisitiza bi. Mshana.

Baraza kupitia Kamati za watumiaji za Mikoa limekuwa likiendesha kampeni ya elimu na usambazaji wa taarifa muhimu zenye maslahi watumiaji kwa lengo la kuongeza uelewa wa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.