Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

​Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Yaundwa Mkoani Shinyanga.


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC) leo Septemba 8, 2026, limeunda Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Shinyanga, ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi wa haki na usalama wa watumiaji wa huduma za mawasiliano, pamoja na kuhakikisha changamoto zinazowakabili watumiaji zinafikishwa katika mamlaka husika kwa ajili ya hatua stahiki.

Kamati hiyo imeundwa na Wajumbe watano wakiwakilisha makundi ya Vijana, wanawake, wajasiriamali, makundi maalumu na wawakilishi wa viongozi wa dini na viongozi wa kata, mitaa na vijiji wakiwa na jukumu la kuelimisha, kuhamasisha na kukusanya maoni ya watumiaji katika ngazi ya mkoa na kuwasilisha kwenye baraza.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya awali kwa wawakilishi Katibu Mtendaji wa TCRA-CCC, Bi. Mary Msuya amesema uundwaji wa kamati unatambulika kisheria lengo likiwa ni kutambua mahitaji ya makundi mbalimbali ya watumiaji wa mawasiliano kupata wawakilishi wa maeneo husika.

“Hadi sasa tumefanikiwa kuunda kamati 22 katika mikoa mbalimbali nchini, ambazo zipo katika mikoa minne ya Zanzibar na mikoa 18 Tanzania Bara, na leo Shinyanga tunaunda kamati nyingine moja ambayo itakuwa ya 23,” amesema Bi. Msuya.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu na Uhamasishaji TCRA-CCC, Bw. Hilary Tesha amesema lengo la kuundwa kwa kamati hiyo ni kuhakikisha wananchi wanafahamu haki na wajibu wao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano, pia inapaswa kuwa sikio kwa kukusanya changamoto za watumiaji na kuzifikisha katika mamlaka husika