Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

WAANDISHI WA HABARI NA WAANDAAJI WA VIPINDI TBC 1 WAPEWA ELIMU KUHUSIANA NA UMUHIMU WA KUPATA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano limewataka watumiaji wa huduma za mawasiliano kuendelea kulitumia Baraza kwani ndio chombo pekee kilichoundwa kwa mujibu wa sheria kulinda,kutetea na kuboresha maslahi ya mtumiaji hivyo basi watumiaji wametakiwa kuendelea kutoa maoni na ushauri pamoja na changamoto zozote wanazokutana nazo wakiwa wanatumia huduma za mawasiliano Nchini.

Akizungumza kwenye semina maalumu ya kuwaongezea uwezo waandishi wa habari na waandaji wa vipindi wa kituo cha kurushia matangazo TBC1 iliyofanyika kwenye Ofisi za kituo hicho Mikocheni Dar es salaam Katibu Mtendaji wa Baraza Mary Shao Msuya amesema’’Ndugu zangu wanahabari nyinyi kimsingi ndio wenye uwezo wa kufikisha maudhui mbalimbali kwa walengwa na tumeamua Kufanya semina hii ya kujengeana uwezo wa kulitambua Baraza pamoja na majukumu yake ili kusudi wakati tunapeleka elimu basi tuwe kwenye mstari mmoja kwakuwa mmeshalijua Baraza la majukumu yake na ikiwezekana kabisa nyie ni mabalozi wa kuendelea kutoa elimu kwa mtumiaji kuhusiana na kutambua haki na wajibu wao na umuhimu wa kupata huduma bora za mawasiliano kwa wote.’’Alisema Shao.

Katibu Mtendaji wa Baraza amesema ili kumfikia mtumiaji na kutimiza ile dhana kulinda maslahi ya mtumiaji Baraza lina kamati za watumiaji wa huduma za mawasiliano ambazo zimeanzishwa kwa sheria ya mamlaka ya mawasiliano ya mwaka 2003,kifungu cha 38 lengo likiwa kuhamasisha watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kuhusu haki na wajibu wao pamoja na kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwenye Baraza.

Mary Shao Msuya amewaomba waandishi wa habari kuendelea kutumia vyombo vyao vya habari na kalamu zao vizuri katika kuendelea kumwelimisha mtumiaji juu ya matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano,lakini pia kutokana na kuongezeka kwa fursa nyingi katika matumizi ya huduma za mawasiliano bado,tunaona kuna utapeli wa kimtandao hivyo basi jamii. ‘’Ifike mahali tuseme basi na tuwe na uwezo wa kujilinda. na elimu hiyo tumeendelea kuitoa kwa kukutana na wadau mbalimbali kwenye maonesho ambayo huwa tunashiriki,kupitia vyombo vya habari,mitandao ya kijamii lakini pia kwa sasa Baraza limefungua TCRA CCC Online Tv ambapo mtumiaji atapata matukio yote ya Baraza huko.