Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI SIMIYU WAPEWA ELIMU JUU YA ULINZI WA MTOTO MTANDAONI.


Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Simiyu wametoa elimu juu ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni katika shule ya Sekondari ya Simiyu iliyopo kata ya Malambo Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza kwa niaba ya wanakamati Katibu wa kamati hiyo David Wambura amesema takribani wanafunzi mia tano wamefikiwa na kupewa elimu juu ya ulinzi wa mtoto mtandaoni wakiwemo wanafunzi wa kidato cha pili na wanafunzi wa kidato cha nne.

Faustine Gomu Mwenyekiti wa kamati ya watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Simiyu ameongeza kwa kusema wamelenga wanafunzi wa shule za sekondari kwasababu wanajiandaa kuwa watu wazima yaani kufikisha umri wa miaka kumi na nane.

Aidha Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema wameona kuendelea kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano kwa wanafunzi kwakuwa bado hawazitambui na somo hili linahitajika sana hasa kipindi hiki ambacho tunashuhudiamabadiliko makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano na kuongeza kuwa utaratibu huu ni endelevu ikiwa ni majukumu ya kila siku ya kiutendaji ya kamati.