Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

TCRA Consumer Consultative Council (TCRA-CCC)

Corporate logo

News

WANUFAIKA WA TASAF WAPIGWA MSASA JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA HUDUMA ZA MAWASILIANO


Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) wakiwa na jukumu kubwa la Kisheria kuanzisha na kusimamia Kamati za Watumiaji wa huduma za Mawasiliano katika Mikoa mbalimbali zenye jukumu kubwa la kukusanya na kuwakilisha maslahi ya watumiaji katika Mikoa lengo likiwa ni kutimiza kauli mbiu ya Baraza inayosema Huduma Bora ya Mawasiliano ni Haki Yako.

Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Mkoa wa Kigoma imeendelea kugusa maslahi ya watumiaji kwa kutoa elimu kuhusiana na umuhimu wa kujilinda na utapeli wa mitandaoni kwa walengwa wa TASAF.

Wakizungumza mara baada ya kupokea elimu hiyo wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF wameshukuru Kamati kwa kuwapelekea elimu juu ya matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano kwa kuwa ni dhahiri kuwa kutokana na ukuaji wa Teknolojia ya habari na mawasiliano duniani kumekuwa na changamoto kubwa ya matumizi yasiyo sahihi ya mawasiliano hali iliyopelekea kuongezeka kwa vitendo vya utapeli mtandaoni hivyo wameomba Baraza kuendelea na mkakati kabambe kuwafikia watumiaji wengi zaidi.

Kamati za Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano zimeanzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003, Kifungu cha 38. Lengo la kuanzishwa kwa kamati za watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano ni kuhamasisha watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano nchini kuhusu haki na wajibu wao; pamoja na kukusanya maoni na kero za watumiaji na kuziwasilisha kwa Baraza.